Kongamano la Bantu 11

Matangazo na miito

Mwito wa pili

Wito wa ikisiri za mawasilisho kwa Mkutano wa 11 wa Kimataifa wa Lugha za Kibantu (Bantu 11) katika Chuo Kikuu cha Ghent (Agosti 18-21, 2026) sasa umefunguliwa. Mkutano huo utajumuisha kikao kikuu kinachokaribisha mawasilisho kuhusu kipengele chochote cha lugha za Kibantu, pamoja na warsha kumi na moja zinazohusika mada maalum (tazama maelezo ya warsha hapa).

Tarehe ya mwisho kwa ikisiri ya mawasilisho ni Desemba 8, 2025 (23:59 UTC/GMT+1). Kila mtu anapaswa kutoa ikisiri zisizoongeza mbili na moja kati yake tu iwe ya mtu peke yake. Ikisiri iwe na ukurasa 1 wa maandishi (ikiwemo takwimu/jedwali/mifano ya lugha) na ukurasa 1 wa ziada kwa marejeleo, katika fonti ya Charis SIL ya pt 11 au fonti ya Times New Roman ya pt 12, yenye nafasi moja, yenye pembezoni mwa kawaida za A4 (cm 2.54). Mawasilisho yanaweza kutolewa ana kwa ana au mtandaoni. Kutakuwa na ada ya mkutano iliyopunguzwa kwa wanafunzi (ikiwemo wanafunzi wa PhD) na washiriki kutoka nchi zenye kipato cha chini.

Lazima ikisiri ipelekwe kupitia jukwaa la EasyAbs tu. Kama bado huna akaunti ya EasyAbs, utengeneze kwanza akaunti ya bure kwenye EasyAbs, kisha upeleke ikisiri yako kwenye mkutano wa Bantu 11, ukifuata miongozo ya uumbizaji hapo juu. Tafadhali hakikisha kwamba faili ya muhtasari (ikiwa ni pamoja na jina la faili) isiwe na jina na iwe katika muundo wa .pdf. Tafadhali ongeza alama ya warsha husika (k.m. ‘WS01’) au tumia ‘GS’ kwa wasilisho la kikao kikuu, na ongeza maneno muhimu 3-5 yanayoelezea wasilisho lako (k.m. ‘fonolojia’, ‘sociolinguistics’, ‘Southern Bantu’). Ikiwa unalipeleka wasilisho lililoandikwa na mtu mmoja, tafadhali onyesha ikiwa unatarajia kuwepo Ghent. Ikiwa unalipeleka wasilisho lililoandikwa na zaidi ya mtu mmoja, tafadhali onyesha ni waandishi wangapi wanatarajia kuwepo Ghent.

Ikiwa una matatizo yoyote na jukwaa la EasyAbs, jaribu kuonyesha upya ukurasa, tumia programu tofauti ya mtandaoni, angalia tovuti ya EasyAbs (https://easyabs.linguistlist.org/about/), au wasiliana na kamati ya maandalizi ya Bantu11 kwa Bantu11@UGent.be.

Taarifa zaidi zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya mkutano. Maswali yote yanaweza kutumwa kwa Bantu11@UGent.be.

Tarehe muhimu zijazo:

  • Desemba 1, 2025 Desemba 8, 2025: tarehe ya mwisho ya ikisiri za mawasilisho
  • Januari 20, 2026: arifa za kukubalika
  • Februari 15, 2026: ufunguzi wa usajili (mapema hadi Aprili 1)
  • Juni 15, 2026: tarehe ya mwisho ya usajili
  • Agosti 18-21, 2026: tarehe za mkutano

Tunatarajia kupokea ikisiri zenu na kuwakaribisha nyote Ghent!

Mwito wa kwanza

Tovuti ya Kongamano la Bantu11 iko mtandaoni sasa. Hapa utapata habari muhimu zote ambazo zitasasishwa mara kwa mara. Kwa sasa, inakufahamisha kuhusu mahali pa Kongamano na tarehe muhimu za kukumbuka.

Tarehe ya mwisho ya kwanza ni 15 Oktoba 2025 (23:59 UTC/GMT+2), kwa ajili ya kutoa mapendekezo ya warsha. Tutumie kwa Bantu11@UGent.be kufikia wakati huo ikisiri yako yenye maneno yasiyozidi 1000 yakiwemo marejeleo na mstari wa kwanza wa sentensi za mifano ya lugha. Tafadhali taja majina ya wasimamizi wa warsha, lakini USIJUMUISHE orodha ya mawasilisho/wawasilishaji. Tutachapisha warsha zilizochaguliwa kwenye tovuti ya Kongamano kabla ya tarehe 1 Novemba 2025.

Tarehe ya mwisho ya pili kwa ikisiri ya mawasilisho, ni tarehe 1 Desemba 2025 (23:59 UTC/GMT+2). Utoaji wa ikisiri utafunguliwa kuanzia tarehe 1 Novemba hadi tarehe hii ya mwisho. Tafadhali usitutumie mapendekezo yoyote ya wasilisho kabla ya kipindi hiki, ili uweze kutujulisha kama unataka kushiriki katika warsha au katika kikao cha jumla. Maelezo zaidi kuhusu utaratibu wa utoaji wa ikisiri utafuata baadaye.

Mahali pa mkutano patakuwa Chuo cha Ledeganck karibu na Makumbusho ya Chuo Kikuu cha Ghent na Bustani ya Mimea. Chuo hiki kiko karibu na kituo cha Gent-Sint-Pieters, kituo kikuu cha treni cha jiji, ambacho kimeunganishwa moja kwa moja na Uwanja wa Ndege wa Brussels na kinachoweza kufikiwa kutoka kwa vituo vikuu vyote vya treni vya Ulaya, ikiwemo kituo cha Leiden (Uholanzi), ambapo Kongamano la 55 la Lugha na Isimu za Kiafrika (CALL 2026) litafanyika kuanzia tarehe 24 Agosti hadi 2026 Agosti. Jiji pia lina kituo cha Flixbus karibu na kituo cha gari moshi cha Gent Dampoort, ambacho kimeunganishwa vyema na miji mikubwa ya Ulaya, ikiwemo Rotterdam na The Hague, ambapo kuna matreni yaelekeayo Leiden.

Tafadhali bofya hapa kwa kuona mahali pa kukaa palipo karibu Chuo cha Ledeganck. Kwa mahali pa kukaa pengine na mambo ya kufanya, tafadhali tembelea tovuti ya Tembelea Gent.

Tunatazamia kupokea mapendekezo yenu ya warsha na kuwakaribisha nyote Ghent!

Tangazo la kwanza

Timu ya BantUGent ina furaha kukukaribisheni jiji la Ghent (Ubelgiji) kwa Kongamano la 11 la Kimataifa la Lugha za Kibantu (Bantu11). Litafanyika kuanzia Agosti 18 hadi Agosti 21, 2026, kabla tu ya Kongamano la 55 la Lugha na Isimu za Kiafrika (CALL 2026) huko Leiden (Uholanzi) kuanzia Agosti 24 hadi Agosti 26, 2026. Mwito wa kwanza wa mawasilisho na warsha utatangazwa mwezi mwa Septemba 2025. Mkiwa na maswali tafadhali yatume kwa anwani ifuatayo: Bantu11@UGent.be.

Mahali

Mkutano wa Bantu 11 utafanyika Chuo cha Ledeganck karibu na Makumbusho ya Chuo Kikuu cha Ghent na Bustani ya Mimea. Chuo hiki kiko karibu na kituo cha Gent-Sint-Pieters. Madokezo ya mahali pa kukaa karibu na Chuo cha Ledeganck yanapatikana hapa. Mahali pengine pa kukaa na mambo ya kufanya jijini yanapatikana kwenye tovuti ya Tembelea Gent.

Tarehe muhimu

  • Oktoba 15, 2025: tarehe ya mwisho ya warsha
  • Novemba 1, 2025: tarehe ya tangazo la warsha zilizochaguliwa
  • Desemba 1, 2025: tarehe ya mwisho ya mawasilisho
  • Januari 15, 2026: arifa za kukubalika
  • Februari 15, 2026: ufunguzi wa usajili (wa mapema hadi Aprili 1)
  • Juni 15, 2026: tarehe ya mwisho ya usajili
  • Agosti 18-21, 2026: tarehe za mkutano

Warsha

Mkutano wetu utajumuisha kikao cha jumla ambacho kitakaribisha mawasilisho kuhusu kipengele chochote cha lugha za Kibantu, pamoja na warsha zifuatazo:

Programu

Itatangazwa baadaye.

Fomu ya usajili

Itatangazwa tarehe 15 Februari 2025

Ada za usajili

Zitatangazwa baadaye.

Kamati ya maandalizi

Paulin Baraka Bose

Arnaud Bizongwako

Koen Bostoen

Pieter De Coene

Maud Devos

Sebastian Dom

Heidi Goes

Hilde Gunnink

Mawasiliano

Ututumie barua pepe kwa njia ya Bantu11@UGent.be.

Elisabeth Kerr

Lorenzo Maselli

Edward Ntonda

Sara Pacchiarotti

Chrisnah Renaudot Mfouhou

Nina van der Vlugt

Aron Zahran